Swahili

Tarehe 22 Oktoba 2013, Tandem Law walikuwa wakili katika kikundi cha kulipa fidia(Group Litigaton Order, GLO) kwa madai dhidi ya Uingereza na Ofisi ya Common Wealth na serikali.

GLO inahusika na matukio yaliyotokea nchini Kenya mnamo tarehe 20 Oktoba 1952 hadi 12 Decemba 1963. Inatambuliwa kama, Kenya Emergency Group Litigation yaani, “kikundi cha madai dharura nchini Kenya.

Tandem Law inawakilisha maelfu ya waliohasiriwa kwenye tukio hili. Mtu yeyote anayetaka kugiunga na kikundi hichi cha madai lazima ajisajili kujaza fomu iliyoko upande wa kuliya. Siku ya mwisho ya kuleta mada ni saa kumi jioni tarehe 30 Aprili 2014 saa za Uingereza. Hakuna mlalamishi yeyote ataruhusiwa kujiunga na kikundi baada ya tarehe ya kufunga, ila kwa ruhusa kutoka kotini.

Kiungo cha notisi kwa ujumla kinapatikana mwisho wa ukurasa huu.

Mawasiliano

Ukiwa ta tashwishi yeyote kuhusu madai, tafadhali wasiliana na mawakili wenzetu walioko Kenya.

Cecil Miller Advocates imechaguliwa kuwakilisha Tandem Law nchini Kenya kuhusiana na , Kenya Emergency Group Litigation yaani, “kikundi cha madai dharura nchini Kenya.

Cecil Miller Advocates in miongoni mwa mawakili wanaoongoza nchini Kenya na wanasifika sana kwa kazi yao ya kuwakilisha matukio kwenye koti za Kenya. Tandem Law ni kikundi cha mawakili walioko Uingereza wanao wakilisha madai haya.

Cecil Miller

Miller & Company Advocates

Standard Street

Bruce House, 13th Floor

P.O. Box 45707 - 00100

Nairobi

 

Tel: +254 20 2248461, 2248467, 2228081

Cell: +254 727 531005, 736 248424

Fax: +254 20 2249754

 

Taarifa na Matukio

Bonyeza hapa kupata tarifa kamili ya notisi

Kusoma taarifa kamili kuhusu mchakato wa fidia bonyeza hapa.